IMEBAINIKA kuwa ile ndoa ya mwanamuziki wa kitambo ndani ya Bongo Fleva,
Luten Kalama ilivunjika miaka mingi iliyopita chanzo kikitajwa ni
mpenzi wake wa sasa Isabela Mpanda.
Kwa mujibu wa chanzo makini, ndoa ya Kalama na mkewe Shufaa iliyofungwa
mwaka 1998 haikuwa na uhai kwani miaka michache baadaye, walitofautina
ingawa hawakuweka wazi ugomvi wao.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, wanandoa hao walikuwa wakigombana mara kwa
mara huku mwigizaji, Isabela akitajwa kuwa chanzo cha kuvunjika.
Mpekuzi wetu alimtafuta Kalama ili kujua uhai wa ndoa yao ambapo alikiri kuvunjika na kusema kwa sasa yupo na Isabela.
Kwa upande wa Isabela alipoulizwa kuhusika kuivunja ndoa hiyo, alisema:
“Heh! Kalama na mimi damdam. Chezea Kalama wewe, kanitoa usichana ati
Kwa hiyo mlitaka mimi ndo niachike. Siwezi kumuacha miaka mia nane''
No comments:
Post a Comment