Siku moja tangu big boss wa Mtanashati Entertainment kutangaza kumtimua aliekuwa manager wa crew hiyo aitwaye Maneno John huku Maneno akidai kuwa yeye ndiye aliyeamua kujitoa mwenyewe kundini, kimenuka mbayaa na ostaz ameamua kusimama kidete
Infoz toka kwa Ostaz Juma na Msoma ni kwamba Maneno anasakwa na polisi kwa udi na uvumba kujibu kesi ya ‘wizi wa kuaminiwa na kutishia kwa maneno‘.
“Hapa navyoongea ni kuwa tayari nimefungua kesi kwenye kituo cha polisi huku Mbezi ya Kimara na nimepewa RB yake namba RB 10404/2012 ambayo inatokana na kuniibia milioni 1.7 iliyokuwa ya kununulia mavazi ya wasanii wangu lakini kila nilipokuwa nikimuuliza alikuwa akiuma uma maneno na baada ya kuchunguza niligundua kazitumia kwa matumizi yake binafsi“ alionisanua Ostaz Juma na Musoma.
“Tangu jana nimekuwa nikimpigia simu ili aje tumalizane hapokei, nimeenda kwake hayupo na pia amepigiwa simu mara kibao na mkuu wa kituo cha polisi Mbezi pale lakini hapokei sijui anataka nini.Nachotaka kuwaambia Watanzania ni kuwa Mtanashati Ent. itahakikisha Maneno anafikishwa mahakamani kujibu shitaka hili, na hapa ndipo atakapojifunza nidhamu ya kufanya kazi proffessionally“,alimalizia Ostaz Juma
Kuhusu suma yeye ameondolea kwenye kundi kutoka na na tabia za kihuni na uchonganishi kwenye kundi ''suma kwangu ni kama mdogo wangu ila tabia ambazo alizileta kwenye kundi sikuridhika nazo kama ulevi,kuzusha zusha meneno nimeona na yeye atasumbua baadae''alimaliza Ostaz juma na musoma
No comments:
Post a Comment